Saturday, July 20

Mawifi wamliza mke wa Tambwe, Yanga, Simba gumzo

0


By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mke wa Tambwe Raiyan Mohammed aliingia ukumbini saa 3:30 usiku akisindizwa na muziki wa taarabu kutoka kwa bendi ya Halichachi Modern Taarabu kwenye ukumbi wa CCM Ilala Boma jijini Dar es Salaam.

Mshehereshaji (MC) Amina Msagasumu mke wa mwanamuziki wa singeli, Msaga Sumu aliwataka wageni kusimama na kumpokea bibi harusi kwa shangwe.

Baada ya kuingia Ray wa Tambwe alishidwa kuvumilia baada ya kudondosha chozi ukumbini wakati akiwatambulisha wageni.

Tukio hilo lilitokea wakati anawatambulisha mawifi zake ambao wamefunga safari kutoka Burundi hadi Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli hiyo.

Raiyan alianza kuwatambulisha wazazi wake mama yake mzazi na mama mlezi wake.

Alifanya tukio hilo pia wakati wa kuwatunza wazazi wake hao.

Yanga, Simba wafunika sherehe ya Tambwe

Klabu za Simba na Yanga zimetokea kwenye sherehe za usiku wa zawadi wa Amissi Tambwe.

MC ambaye ni mke wa Msagasumu alimtambulisha Tambwe kwa kusema mchezaji wa zamani wa Simba na baadaye wa Yanga.

Ndipo kelele za nguvu zikaibuka ambapo wa Simba walikuwa wa kwanza kufika kwenye steji na kufanya mambo yao, yaani walicheza mwanzo mwisho.

Ilipofika kwa mashabiki wale wa Yanga walipoitwa na MC walikuwa wakishangilia chini hawakupanda stejini na ikawa mwisho.

Tambwe ambaye ni mshambuliaji awali aliichezea Simba na baadaye akajiunga na Yanga anayoichezea mpaka sasa.

Unapoingia ndani kuna studio mbili moja upande wa kushoto wa kupiga nyimbo za wasanii na kulia ni mubashara ‘live’ wa bendi ya Halichachi Modern Taarabu.

Wataalamu wa muziki huu wamekuwa wakipeana zamu ya kupiga ambapo ulianza wa kurekodi na sasa ni mubashara.

Sherehe ya leo ni mwendelezo wa nyingine zilizopita ambapo ilianza ya Singo na baadaye ikafuata ndoa.

Muziki unaopigwa katika shughuli hii ni wa Taarabu kwa sehemu kubwa ndiyo imetawala ukumbini hapa.

Share.

About Author

Leave A Reply