Thursday, February 21

Mastaa wanne Stars kutua kambini

0


By CLIFORD NDIMBO, TFF

TIMU ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaendelea na maandalizi yake ya mchezo wa kuitafuta tiketi ya kufuzu Afcon 2019 dhidi ya Lesotho utakaochezwa wiki ijayo mjini Maseru, Lesotho.
Katika mazoezi ya timu hiyo iliyopo Afrika Kusini, kipa Beno Kakolanya na mshambuliaji chipukizi, Yahya Zayd walipumzishwa baada ya kugongana.
Hata hivyo, taarifa ya madaktari wachezaji hao wataendelea na mazoezi kuanzia kesho Jumamosi.
Wanaotarajiwa kuanza kuripoti ni mabeki Ramadhan Kessy (Nkana, Zambia), Himid Mao (Petrojet,Misri) na Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini) sambamba na straika Rashid Mandawa (BDF, Botswana).
Nyota wengine waliobaki akiwamo Simon Msuva (El Jajida, Morocc0), Farid Mussa na Shaaban Idd (Tenerife, Hispania) wataripoti kuanzia Novemba 12,2018.

Share.

About Author

Leave A Reply