Thursday, February 21

Masau Bwire aigeuzia kibao Stand United, yapapaswa 2-1

0


Timu ya Ruvu Shooting imeondoa gundu la kupoteza mechi kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kuirarua Stand United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Ushindi huo umefuta mkosi kwenye kikosi hicho ambacho michezo yake miwili iliyopita ilijikuta ikishindiliwa jumla ya mabao 9.

Mchezo wake dhidi ya Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, ilijikuta ikitandikwa mabao 5-1 kisha mchezo uliofuta ikatulizwa kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.

MATOKEO MECHI ZOTE ZA LEO JUMATANO:

Alliance FC 1-0 Mtibwa Sugar.

Mwadui FC 1-0 Lipuli FC.

Ruvu Shooting 2-1 Stand United.

Kagera Sugar 1-1 Singida United.

Coastal Union 1-0 Ndanda SC.

Biashara United 0-0 Tanzania Prisons.

Share.

About Author

Leave A Reply