Wednesday, August 21

Manula kutetea mataji yake

0


By Thobias Sebastian

KIPA namba moja wa Simba na Taifa Stars, Aishi Manula ameweka hadharani mafanikio yake ya kutwaa tuzo mfululizo kwani yamechangiwa na jinsi anavyojituma.
Msimu uliopita ulikuwa msimu wake wa kwanza kucheza Simba akitokea Azam lakini alitwaa tuzo ya kipa bora wa Simba kwenye tuzo za Mo Simba Awards huku akinyakuwa pia tuzo ya kipa bora wa ligi nzima.
Manula alisema msimu huu umekuwa mzuri kwake na timu kwa ujumla kwa maana ya kutimiza malengo ya kufika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe.
“Mafanikio mengine ya timu ambayo tumefanikiwa ni kuchukua ubingwa wa ligi ambayo umetupa tena nafasi ya kucheza mashindano ya Kimataifa msimu ujao,”
“Msimu mzuri kwangu kutokana nimeweza kuwa chaguo la kwanza kwenye timu lakini kuchukua tena tuzo hii kama ilivyokuwa msimu uliopita lakini nisingeweza kufanya hivi bila ya ushirikiano kutoka kwa kaka yangu Deo Munishi ‘Dida’.
“Malango yangu yanaweza kutimiza zaidi pale ambapo nitatetea tena tuzo yangu ya kipa bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu kama ambavyo nilichukua msimu uliopita,” alisema Manula


Share.

About Author

Leave A Reply