Sunday, August 18

Manchester United yashikwa na Chelsea, Ligi ya Mabingwa Old Trafford shaka tu

0


Manchester, England. Uzembe wa kipa David de Gea ulitoa nafasi kwa Marcos Alonso kufunga bao la kusawazisha Chelsea ikipara sare 1-1 na Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Wenyeji Manchester United walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wake Juan Mata katika dakika 11 ya mchezo.

Matokeo hayo yanaiweka vizuri Chelsea katika nafasi ya kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa huku Manchester United ikijiweka njia panda.

Wakati Man United ikiongoza kwa bao Juan Mata dhidi ya timu yake ya zamani, lakini uzembe wa De Gea alipokuokoa vizuri shuti la Antonio Rudiger la umbali wa mita 30, lilitoa mwanya kwa Marcos Alonso kumalizia wavuni kwa ufundi mkubwa.

Hadi wakati Chelsea inasawazisha, Man United ilikuwa ikitawala mchezo huo, lakini matokeo hayo yamewafanya wenyeji kubaki katika nafasi ya sita wakiwa nyuma kwa pointi tatu kwa Chelsea inayoshika nafasi ya nne ikiwa na mechi mbili mkononi.

Katika mchezo mwingine wa ligi, Arsenal iliendelea kuteseka na kujiweka pagumu zaidi katika harakati zao wa kuwamo ndani ya Top Four ya Ligi Kuu England msimu huu baada ya Kukumbana na kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Leicester City.

Kikosi hicho cha Unai Emery kimeendelea kuwa na rekodi mbovu kwenye mechi za ugenini baada ya kukubali wavu wao kuguswa mara tatu, ikiwa ni mechi ya tatu mfulululizo kupoteza kwenye ligi hiyo, ambapo mabao mawili ya Jamie Vardy na moja la Youri Tielemans yalitosha kulizamisha jahazi la Arsenal na hivyo kuzidi kujiweka pabaya kwenye mbio za Top Four.

Katika mchezo huo, Arsenal ilichapwa pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wao wa pembeni, Ainsley Maitland-Niles kuonyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza.

Share.

About Author

Leave A Reply