Tuesday, March 19

Man United, Arsenal zaonyeshana ubabe! Chelsea hoi

0


Kocha Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga jambo amablo limesababisha timu hiyo kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal jana Jumatano usiku.

Matokeo hayo yameiweka Manchester United kwenye ushindani kuwapo kwenye timu nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Makosa ya David de Gea na Marcos Rojo  yaliigharimu timu yao jambo ambalo limemfanya Mourinho kuwatupia lawama wachezaji wake.

Licha ya Manchester United kupewa sapoti na mashabiki kwenye uwanja wake wa nyumbani, Arsenal ndio walianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao kupitia kwa Shkodran Mustafi (26’) huku Anthony Martial akiisawazishia United (30’).

Alexandre Lacazette aliwainua mashabiki dakika ya 68’ huku bao hilo likidumu kwa dakika moja tu ambapo Jesse Lingard aliisawazishia Manchester United mnamo dakika ya 69’.

Matokeo mengine kwa mechi zilizopigwa jana usiku

Everton 1-1 Newcastle United

Fulham 1-1 Leicester City

Wolverhampton Wanderers 2-1 Chelsea FC

Tottenham Hotspur 3-1 Southampton

Share.

About Author

Leave A Reply