Friday, July 19

Man City yamaliza ubishi kwa Man United, Arsenal..

0


MANCHESTER, ENGLAND
Kikosi cha Manchester United kimeshindwa kutamba mbele ya watani wao Man City baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Etihad.
Man City walianza kung’ara mwanzoni kabisa mwa mchezo na dakika 12, walipachika bao kupitia kwa David Silva, akimalizia
mpira uliopigwa na Bernado Silva.
Wakati Manchester United wakipokea kichapo hicho, kiungo wao Mfaransa Paul Pogba alikuwa jukwaani akitazama mechi hiyo kama mtazamaji.
Man City waliongeza bao la pili dakika ya 48, likifungwa na Sergio Aguero ‘Kun’, wakati wanajipanga Manchester United
walipambana na kupata bao pekee dakika ya 58, likifungwa kwa njia ya penalti na Anthony Martial. Bao la tatu la Manchester City lilipachikwa na Ilkay Gundogan dakika ya 86.

MICHEZO MINGINE
Wagonga nyundo wa Arsenal walishindwa kutamba kwenye dimba lao la Emirates na kumaliza kwa sare ya 1-1, na Wolverhampton Wanderers wakati Chelsea imetoka suluhu mbele ya Everton. Mchezo wa Chelsea Wolver ulipigwa Uwanja wa Stamford Bridge.
Kwa upande wa Liverpool wao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Fulham.

Share.

About Author

Leave A Reply