Monday, March 25

Magufuli ateua wengine

0


By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais John  Magufuli amemteua Jaji mstaafu Steven Bwana kuwa mwenyekiti wa Tume ya  Utumishi  wa Umma kwa kipindi  cha miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Desemba 4, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa pamoja na kumteua Bwana, Rais Magufuli amewateua makamishna watano wa tume hiyo.
Walioteuliwa ni  George Yambesi, Balozi  mstaafu  John Haule,  Immaculate Ngwale, Yahaya Mbila na Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay.
Inaeleza kuwa uteuzi wa mwenyekiti wa makamishna wa tume hiyo umeanza Novemba 22, 2018.

Share.

About Author

Leave A Reply