Saturday, August 24

Magufuli arejea nchini baada ya kukamilisha ziara

0


By Aurea Simtowe, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amerejea nchini leo Alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kufanya ziara nchini Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia na Malawi.

Amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Rais Magufuli akiwa Zimbabwe alifanya ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Kabla ya kufanya ziara nchini Zimbabwe, Magufuli alikuwa   Afrika Kusini ambako pamoja na kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa, alifanya naye mazungumzo

Baada ya kutoka Afrika Kusini alielekea  Namibia ambako alifanya ziara ya kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Hage Geingob.

Akiwa Namibia alifungua mtaa uliopewa jina la Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere pamoja na kutembelea eneo walilozikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia na kiwanda cha nyama cha Meatco.

Share.

About Author

Leave A Reply