Friday, July 19

Magereza waanza kutekeleza agizo la Magufuli

0


By Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Magereza 10 nchini Tanzania zimethibitishwa kutumika katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.

Rais Magufuli  aliagiza Jeshi la Magereza kuwatumia wafungwa kuzalisha  mazao ya biashara na chakula badala ya Serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.

Akizungumza leo Novemba  24, 2018 katika Gereza la Kwamngumi mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini.

Amesema upo mpango maalumu wa kutathmini na kupima mkakati huo kwa kila gereza.

Ametaja magereza hizo kuwa ni Songwe (Mbeya), Kitai (Ruvuma), Ludewa (Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera),  Idete na Kiberege (Morogoro), Kitete (Rukwa), Kwangumi na gereza la Arusha.

“Lengo la wizara kupitia Jeshi la Magereza ni kuwekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi na ikiwezekana hapo baadaye tutafuta wateja watakaonunua mazao tutakayozalisha,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, amesema wamejipanga vizuri kutekeleza agizo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.

 

Share.

About Author

Leave A Reply