Sunday, August 25

Lukumay, Lingalangala wakubali yaishe tu

0


By Imani Makongoro

WAKATI Kesho Jumanne kampeni rasmi za uchaguzi wa klabu ya Yanga zikianza, wagombea 14 kati ya 15 walioenguliwa kwenye usaili wamejiondoa rasmi katika uchaguzi huo.

Licha ya wagombea hao kuenguliwa, walipewa siku tatu kwa ajili ya kukata rufani kupinga kuenguliwa kwao na ni mmoja pekee ambaye amekata rufani.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela amesema mgombea aliyekata rufani kupinga kuenguliwa kwake ni Rodgers Gumbo.

Gumbo anayegombea nafasi ya ujumbe alienguliwa kwa kigezo cha kutokuwa na uzoefu wa kutosha.

“Rufani yake itasikilizwa Aprili 30 (kesho) na kutolewa uamuzi siku hiyo hiyo,” alisema Mchungahela.

Wagombea wengine walioongeliwa kwenye usaili na wameridhika na uamuzi huo na sababu za kuenguliwa kwao kwenye mabano ni Lucas Mashauri (hakuhudhuria usaili).

Wengine ni Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika (waliwekewa pingamizi la kutowasilisha ripoti ya mapato na matumizi walipokuwa wajumbe wa kamati tendaji ya Yanga iliyopita).

Pia Ally Sultan ‘Chota’ (hakuambatanisha nyaraka muhimu), Seko Kingo (hana uzoefu wa kutosha), Cyprian Musiba (hakuhudhuria usaili), Dk Nasoro Matuzya (amefungiwa na BMT), Abdallah Chikawe (hakuambatanisha nyakara muhimu), Said Omar ‘Ntimizi’ (hakuhudhuria usaili), Palina Conrad (hana uzoefu wa kutosha), Mkumbo Mkoma (hana uzoefu) na Seif Hassan (hakuambatanisha nyaraka muhimu).

Wagombea hao walipewa muda wa kukata rufani kupinga kuenguliwa kwao kwa siku tatu kuanzia Aprili 24 hadi 26 na kuanzia Aprili 27 hadi leo Jumatatu rufani zao kusikilizwa.

“Ni Rogars pekee ambaye amekata rufani na atasikilizwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF Jumanne ijayo (kesho) na matokeo yatatangazwa siku hiyo hiyo ambapo kampeni rasmi zitaanza,” alisema.

Akizungumzia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama kupinga mchakato wa uchaguzi, Mchungahela alisema hakuna kesi hiyo na kama ipo basi itaendelea upande mmoja.

“Kesi iliyokuwapo ilikuwa ni ya kutumia kadi za wanachama, tuliambiwa tufuate utaratibu, sababu kadi ambazo ziligomewa na wanachama ni kadi za mwendo kasi (kadi za benki), sisi hatutumii hizo kadi tunatumia leja ya klabu.”

Share.

About Author

Leave A Reply