Sunday, August 25

Linah na Amin wanasa Msitu wa Magamba

0


By Elizabeth Edward

Kama unafuatilia mitandao ya kijamii utakuwa umekutana na picha kali za mastaa Amin na Lina wakiwa katika mandhari ya kuvutia.

Picha hizo zimezua gumzo ikizingatiwa kuwa wawili hao waliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, wengi wakijiuliza kama kweli wameamua kulirudisha penzi hilo lililovunjika miaka mingi iliyopita.

Ukweli ni kwamba wawili hawa walikuwa ‘location’ wakitengeneza video ya wimbo wao mpya unayofahamika kama Nimenasa.

Amin amesema wimbo ameamua kufanya video hiyo kwenye msitu wa Magamba uliopo wilayani Lushoto baada ya kuvutiwa na mazingira yake na amekuwa na shauku ya kutangaza kivutio hicho cha utalii.

“Nilizungumza na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa ajili ya kupata location nashukuru wamenisaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha video hii na nina uhakika itakuwa miongoni mwa kazi nzuri za mwaka huu.”

“Yaani sioni haja ya kwenda nje ya nchi na niwashauri wasanii wenzangu tutangaze vya kwetu maana kila tunachokifuata huko nje ya nchi hata hapa kwetu vipo tena vizuri zaidi, kule Magamba kuna maporomoko ya kuvutia mno,” amesema Amin.

Mhifadhi Mkuu wa Msitu wa Magamba, Getrude Nganyagwa amewaita wasanii wengi zaidi kwenda kutembelea na kufanya kazi zao kwenye msitu huo wenye vivutio lukuki.

Amesema, “ Nina imani Amin na Lina watakuwa mabalozi wazuri kuwaelezea watanzania walivyoviona, wasanii wengine waje Magamba kuna vivutio vingi ikiwemo maporomoko ya maji, ndege, aina tofauti za miti.”

Share.

About Author

Leave A Reply