Saturday, August 24

Kortin kwa kukwepa kodi ya Sh8.1bilioni

0


By Hadija Jumanne na Fortune Francis [email protected]

Dar es Salaam. Mfanyabiashara wa kuuza mafuta ya Petrol, Abshir Afrah (56), amefikishwa Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu ya kukwepa kodi ya Sh8.1bilioni na kutakatisha fedha haramu kiasi cha Sh8.1bilioni

Afrah ambaye ni mkazi wa Nairobi nchini Kenya na raia wa Somalia, anadaiwa kukwepa kodi hiyo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutokana na biashara aliyokuwa anaifanya nchini ya kuuza mafuta ya Petrol.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Mei 22, 2019 na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka matatu kwenye kesi ya uhujumu uchumi namba 41/2019.

Katika shtaka la  kwanza,  Simon alidai kati ya mwaka 2015 na 2018 ndani ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alikwepa kodi ya Sh8,107,509,385.48 kinyume na sheria ya kodi ya mwaka 2015.

Alidai mshtakiwa huyo alishindwa kulipa kodi hiyo ya TRA kutokana na biashara ya kuuza Mafuta ya Petroli aliyokuwa anaifanya hapa nchini.

Katika shtaka la pili, Afrah anadaiwa kati ya mwaka 2015 na 2018, Ofisi  TRA iliyopo jiji hapa, kinyume na sheria aliisababishia hasara ya Sh8.1 bilioni kwa kukwepa kulipa kodi.

Katika hitaka la tatu, wakili Simon alidai mshitakiwa alitakatisha fedha haramu Sh8.1bilioni, huku akijua fedha hizo ni zao la tangulizi la ukwepaji kodi kwa njia ya udanganyifu.

Simon baada ya kusomewa mashtaka hayo,  Hakimu Mtega alimtaka kutojibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi ipate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).

Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayomkabili hayana dhamana kisheria.

Share.

About Author

Leave A Reply