Thursday, August 22

Kocha Stars:Tuna malengo makubwa Afcon Misri

0


By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Wakati kikosi cha Taifa Stars kikitarajiwa kuanza kambi kesho Alhamisi, kocha msaidizi wa timu hiyo, Hemed Morocco amesema wanamalengo makubwa katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Stars imefuzu kwa mara ya pili kucheza fainali hizo ipo kundi moja na timu za Senegal, Kenya na Algeria.

“Tuna malengo ya kufanya maajabu kwenye mashindano hayo na kuwashangaza wengi,” alisema Morocco jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili na kufafanua.

“Tunajua tunakwenda kupambana na timu kubwa Afrika, lakini mbali na maandalizi ya kiufundi kwa wachezaji wetu, pia tutawaandaa kisaikolojia kupambana na timu kubwa.

Alisema wanahitaji kufika mbali kwenye mashindano hayo na waamini hilo litawezekana.

“Kama nilivyosema, Stars ina malengo madhubuti ya kufanya vizuri katika fainali hizo, dhamira ya kufuzu ilikuwa ni tufanye vizuri pia kwenye mashindano.

“Tuna kikosi bora, chenye uchu wa mafanikio hivyo tunaamini tutafanya vizuri,” alisema Morocco.

Stars inayoundwa na wachezaji nyota 39 itaanza kambi kesho Alhamisi kujiandaa na fainali hizo.


Share.

About Author

Leave A Reply