Friday, August 23

KITANUKA TU! Ukinasa meseji kwa bebi wako

0


By RHOBI CHACHA

NI kosa gani kubwa linaloweza kukutenganisha na mpenzi wako daima? Yaani kosa lisilokuwa na msamaha ule wa saba mara sabini?

Waandishi wa vitabu vya uhusiano, wanasosholojia, wacheza sinema, watunga mashairi yenye ladha mbalimbali za kuonya usaliti wamekosa sababu zinazofanana katika kuvunjika kwa mahusiano.

Hii pia imemkuta kwa msanii Diamond kosa lililokosa msahama ni meseji za usaliti kwa aliyekuwa mpenzi wake Zari, uamuzi unaopingwa na baadhi ya wasanii wenzake.

“Namuheshimu Zari ni mzazi mwenzangu, alikuwa wife material, alikuwa anatoka na Peter wa P-Square, niliwahi kukuta sms nikamuuliza. Alikuwa anachepuka pia na mkufunzi wake na alikua anamleta hadi kwangu, lakini sijawahi kufunguka,” Diamond ameiambia Wasafi FM.

Ameendelea kwa kueleza kuwa, “Na ukweli sijawahi kuachwa na Mwanamke, Ukizingua nitakupiga matukio utaondoka mwenyewe”.

Mwanaspoti lilizungumza na baadhi ya wasanii, kuhusu pindi watakapokuta meseji ya mapenzi kwa mpenzi wake nini anafanya?

Ni msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel anasema katika suala la kukuta meseji kwenye simu ya mpenzi wake,huwa anaumizwa lakini anavumilia ila ipo siku anachoka na uvumilivu hizo meseji za mapenzi zikizidi.

“Kiukweli mimi ni mvumilivu sana katika suala la mapenzi na ndio maana unaona sina skendo ya kuwa na huyu au huyu kila wakati,na ukiona imetokea hivyo basi uvumilivu umenishinda

“Sasa hili suala la kukuta meseji katika simu ya mpenzi wangu, huwa naumia lakini navumilia ila hizo meseji zikizidi huwa nachoka na kuachana na huyo mpenzi, sababu naona ni dharau za waziwazi naletewa,” alisema.

Ametamba sana katika filamu za kibongo, kwa upande wake anasema, huwa hawezi kuvumilia akikuta meseji za mapenzi kwa mpenzi wake, anajukutaga na hasira za maamuzi ya kuachana lakini baada ya muda hasira zinamuisha mapenzi yanazidi kusonga mbele

“Weeeeee acha kabisa, huwa nakuaga na hasira mbaya za kisukuma na wakati mwingine najikuta navunja hata simu ya mwanaume, ila baadaye hasira zikiisha huwa maisha ya mapenzi yanaendelea, lakini kiukweli huwa inauma sana”

Msanii wa filamu ambaye pia ni kiongozi wa tamthilia ya Bongo Dar es Salaam inayorushwa Wasafi Tv anasema, yeye anamke nyumbani pamoja na kuishi nae muda mrefu, hakuna kitu kinachouma katika mapenzi hasa ukute meseji ya mapenzi kwa mpenzi wako.

“Sikiliza ndugu hakuna kitu kinauma kama kukuta meseji ya mapenzi kwa mpenzi wako, ukiuona mtu anafurahia kukuta meseji ya mapenzi kwa mpenzi wake ujue huyo hana mapenzi na huyo mtu, yaani pamoja na kuwa na mke wangu nyumbani huwa sikubaliani na hilo zoezi kwa kweli na siku nikimkuta namuacha moja kwa moja, maana naona ni dharau”

Ni msanii wa muziki wa bongo fleva,ni hodari wa kuimba nyimbo za mapenzi, hivi karibuni kaachia wimbo wake mpya unaitwa ‘Nichombeze’, kwa upande wake anasema akikuta meseji ya mapenzi kwa mpenzi wake huwa ananuna kwa muda mrefu bila ya kuongea nae huyo mwanamke na baadae anamrudia kutokana na msamaha atakaoombwa na hilo tukio likijirudia huwa anaachana na huyo mwanamke.

“Hee jamani mapenzi yanauma dada, yaani nikute meseji ya mapenzi kwa mpenzi wangu nichekelee? Mie huwa nanuna lakini baadae tunakaa chini tunaweka sana, ila kosa likijirudia huwa nakaa pembeni kabisa, maana naona kama hakuna heshima.”

Msanii wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya anasema huwa hana tabia ya kupekuwa simu ya mpenzi wake, ila ikitokea kwa bahati mbaya kaona meseji ya mapenzi huwa anaangalia meseji yenyewe iko ya namna gani, akigundua haimridhishi anaachana na huyo mwanaume.

“Yaani kwanza hadi nikuache kwa ajili ya meseji ya mapenzi jua imeniumiza sana, hivyo ndio maana huwa nakwepa sana kupekua simu ya mpenzi wangu sababu nanijua nikikuta meseji ya mapenzi ambayo hainiridhishi huwa nafunga virago nakuacha ujinafsi kabisa”

Share.

About Author

Leave A Reply