Friday, August 23

Kimbunga Kenneth chaua watatu Comoro, mmoja Msumbiji

0


Cabo Delgado, Msumbiji. Kimbunga Kenneth kimetua Msumbiji ambacho kimepiga katika mkoa wa Cabo Delgado na kuing’oa miti na kuharibu mabati huku watu watatu wakifa nchini Comoro na mmoja Msumbiji.

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu mafuriko na maporomoko ya udongo kutokana na mvua kubwa zitakazonyesha mchana kutwa baada ya kutokea kwa kimbunga hicho.

Kimbunga Idai kilipiga nchini Msumbiji pamoja na Zimbabwe na Malawi katikati ya mwezi Machi. Watu wapatao 1,000 walidaiwa kufariki dunia, 600 kati yao wa nchini Msumbiji.

Kimbunga hicho pia kilisababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni mbili. Shirika la misaada la Care linatarajia hali kuwa mbaya zaidi katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Afrika.

Kimbunga Kenneth kilichotua kwa upepo mkali wa kasi ya 220km/h kimesababisha vifo vya watu watatu katika visiwa vya Comoro wakati ambao Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga nchini Msumbiji, inaeleza kwamba takriban watu 30,000 wamehamishwa kutoka maeneo ambayo yalitarajiwa kuathirika na kimbunga hicho.

Share.

About Author

Leave A Reply