Sunday, August 25

Kilichoiponza Serengeti Boys hiki hapa

0


By THOMAS NG’ITU

KELELE zimekuwa nyingi kwa namna ambavyo makipa wa Timu ya Taifa Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ jinsi wanavyokuwa wanafungwa magoli ya kawaida, ishu hiyo imemfanya kipa wa timu ya Taifa Tanzania, Beno Kakolanya kufunguka namna makipa hao wanavyocheza.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya kutembelea ofisi za Mwananchi Communication Ltd zilizopo Tabata, alisema amekuwa akiwafatilia vijana hao lakini changamoto imeonekana kwenye upande wa makipa.

“Kweli makipa huwa tunafungwa kawasababu huwezi muda wote ukawa unaweza kupambana na washambuliaji, lakini makipa wetu wamefungwa magoli mepesi sana, maelekezo yanatakiwa kuongezeka naamini ni wachezaji wazuri kwa umri wao” alisema.

Beno aliongeza hata katika upande wa ushambuliaji muda mwingine wamekuwa wakicheza kwa ubinafsi kutokana na kila mmoja kutaka kuonyesha uwezo wake badala ya timu kiujumla.

“Bado ni vijana wanazidi kukua polepole wanatakiwa waelekezwe namna ambavyo wanatakiwa wafanye kwenye mashindano kama haya, matokeo ndio kila kitu kwa timu halafu hilo la mmoja mmoja linakuja baadae,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply