Saturday, July 20

Kifo cha kichanga chawaweka matatani daktari, watumishi wanne Butimba

0


Mwanza. Watumishi watano akiwamo daktari wa hospitali ya wilaya Butimba jijini Mwanza, wamesimamishwa kazi kutokana na madai ya uzembe uliosababisha kifo cha mtoto aliyezaliwa Novemba 3, 2018.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 7, 2018, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Philis Nyimbi amesema kumekuwepo na malalamiko ya wananchi katika hospitali hiyo yanayotokana na uzembe unaofanywa na  baadhi ya watumishi.

Amesema rushwa na kauli mbaya kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma ni miongoni mwa malalamiko yanayotolewa na wananchi.

Mkuu huyo wa wilaya amechukua uamuzi huo baada ya kupata taarifa za mzazi aliyefika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kujifungua, lakini akakosa msaada.

“Ushahidi upo kutoka kwa wananchi na sasa ngoja sheria ichukue mkondo wake. Kama kweli ni uzembe ulitokea na kusababisha kifo cha kichanga, basi tusilaumiane,” amesema Nyimbi.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni pamoja na daktari anayedaiwa kupokea fedha mkononi bila kutumia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato unaotambuliwa na Serikali sambamba na wauguzi wanne.

Mmoja kati ya wazazi waliokuwa wodini, Shanifa Lukas amesema licha ya hospitali hiyo kupokea wagonjwa wengi kwa siku, kuna tatizo kubwa kwa watumishi hususan wauguzi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa lugha chafu.

“Wakati wa kujifungua ndipo utasikia nesi anakuzomea kama mtoto mdogo. Anadiriki kukuhoji kwamba wakati mkifanya nilikuwepo,” amesema Shanifa

Share.

About Author

Leave A Reply