Saturday, August 24

Kiemba ataka Stars wapelekewe wanasaikolojia

0


By ELIYA SOLOMON

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Amri Kiemba amesema wachezaji wa Taifa Stars wanatakiwa kuandaliwa kisaikolojia kabla ya fainali za mataifa ya Afrika nchini Misri.

Fainali za mataifa ya Afrika Misri zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi, Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu katika miji minne tofauti nchi humo. Kiemba alisema inawezekana wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia waliofanya maajabu katika fainali za mwaka 2012 na waliishangaza Afrika waliandaliwa kisaikolojia.

“Lazima tutambue kuwa mpira unaanzwa kuchezwa kichwani, inatakiwa waandaliwe kisaikolojia halafu tuone namna ambavyo wanaweza kufanya vizuri.

“Wanaweza wasichukue ubingwa lakini wakaonyesha kiwango ambacho kila mmoja wetu atavutiwa nacho,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Simba.


Share.

About Author

Leave A Reply