Monday, March 18

Kenya yataka Ocampo achunguzwe

0


Nairobi, Kenya. Serikali ya kitaifa sasa inataka kiundwe chombo kinachojitegemea, kisicho na upendeleo na huru kuchunguza maofisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na mwendesha mashtaka wa zamani Luis Moreno Ocampo juu ya majukumu yao katika kesi dhidi ya Wakenya sita.

Hii ni kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu Ken Ogeto, ambaye anaongoza ujumbe wa Kenya katika kikao cha 17 cha Bunge la Vyama vya Mataifa (ASP) kuhusu Mkataba wa Roma katika makao makuu ya ICC huko The Hague, Uholanzi.

Desemba 14, 2010, Ocampo aliwataja Wakenya sita kwamba walikuwa na jukumu kubwa katika machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 yaliyosababisha vifo vya watu 1,300 na wengine zaidi ya 600,000 kutawanyika hovyo.

Waliotajwa ni pamoja na Uhuru Kenyatta ambaye wakati wa machafuko alikuwa naibu waziri mkuu. Sasa Kenyatta ni Rais wa Kenya.

Wengine waliotajwa walikuwa Naibu wa Rais William Ruto, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo katika serikali ya Rais Mwai Kibaki, aliyekuwa Mkuu wa Huduma ya Umma Francis Muthaura na Kamishna wa Polisi Meja Jenerali (mstaafu) Hussein Ali.

Kadhalika walitajwa aliyekuwa waziri wa viwanda Henry Kosgey na mwandishi wa habari Joshua arap Sang.

Ogeto alisema kuwa nchi inatarajia unyofu na uwazi juu ya maelezo na asili ya uchunguzi wa Wakenya sita, ikiwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta.

“Malalamiko dhidi ya mwendesha mashtaka mkuu wa zamani hayapaswi kufunikwa chini ya zuria. Kenya inaitaka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka kupeleka malalamiko kwenye taasisi isiyoegemea upande kufanya uchunguzi wa wazi juu ya madai haya,” alisema.

Ogeto aliisisitizia ICC kuhakikisha kwamba matokeo ya uchunguzi utakaokuwa umefanywa yawekwa wazi kwa umma na kuwapa wanachama wa ASP ili waweze kupitia na kufanya maamuzi sahihi.

“Uaminifu wa ICC ni muhimu kwa nchi wanachama ziweze kuwa na imani na mahakama. Tunachukulia uchunguzi huu kwa uzito mkubwa na tunataka ufanyike wazi na kwa haraka ili matokeo haya yatumike kubainisha ushirikiano wetu wa baadaye na mahakama,” alisema.    

Mgogoro baina ya Burundi na Rwanda umeendelea kukua baada ya Rais Nkurunziza kusema kwa uwazi kwamba mwenzake wa Rwanda Paul Kagame alipanga kuing’oa serikali yake katika mapinduzi yaliyoshindwa ya Mei 13, 2015.

Katika barua hiyo, Nkurunziza amemwambia Museveni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa EAC, kwamba “mbali ya ukweli kwamba Rwanda iliandaa na kusimamia mapinduzi ya mwaka 2015, watu waliohusika na wahalifu wengine wameweka makao katika nchi wanayoungwa mkono kuishambulia Burundi; wakivuka mpaka wa Rwanda-Burundi au kupitia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikiwa ni pamoja na kuwapatia usaidizi na nyaraka za kusafiria kuwawezesha kuzunguka katika eneo hili na hata Ulaya.”

Inafahamika kwamba hii si mara ya kwanza katika miaka kadhaa Nkurunziza akizungumzia kile anachokiita “uvamizi wa Rwanda” katika barua alizowaandikia viongozi wa ukanda huu.

Lakini barua ya Ijumaa ilikuwa na maneno makali na nakala zake ziliztumwa kwa Kagame, Uhuru Kenyatta wa Kenya na kiongozi wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ambao wamesisitiza juu ya kukua kwa mgogoro wa usalama huku wanadiplomasia wakijitahidi kuupatia ufumbuzi kwa miaka kadhaa.

Share.

About Author

Leave A Reply