Sunday, August 25

Kelvin John aogelea ofa kibao

0


By CHARITY JAMES

ACHANA na nafasi ya Serengeti Boys kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa vijana habari ya mjini ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Kelvin John ‘Mbappe’ anaoga ofa za kwenda kucheza soka la kulipwa majuu.

Kwa mujibu wa msemaji wa kituo cha Football House ambacho kina mlea nyota huyo, Francis Felician alisema Mbappe tayari ana ofa kutoka katika klabu ya Ajax ambayo walikubaliana kuwa baada ya mashindano ya Afcon ambayo yanaendelea ndio watawapa jibu kama watampeleka huko au la.

Alisema hadi sasa wana ofa zaidi ya 10 na wanaendelea kupokea kutoka klabu mbalimbali lakini hawapo tayari kuweka wazi ni klabu gani kwani hawajajua kama wana maanisha au wanazungumza tu hadi hapo watakapokaa nao meza moja mara baada ya mashindano hayo kumalizika.

“Nimesikia taarifa za kwamba mimi nimemkatalia Mbappe kwenda Ajux sio kweli tuliingia katika makubaliano na viongozi wa hiyo timu kuwa tutafanya maamuzi ya wapi atakapoenda baada ya Afcon na waliliheshimu hilo na sisi msimamo wetu upo palepale,”

“Kelvin ni kijana mdogo ndio kwanza anatafuta maisha na soka ndio ajira yake hivyo tunaendelea kuangalia timu ambayo itakuwa na masklahi mazuri zaidi kwake ndiyo tutakayompeleka pia katika mashindano yanayoendelea tayari tumepokea ofa nyingine lakini bado hatujakaa mezani na viongozi wa izo timu siwezi kukwambia ni zipi hadi hapo nitakapokaa nao,” alisema.

Alisema pia wana mialiko mingi ya majaribio kutoka nchi ambazo zinafanya vizuri kimpira lakini ugumu unabaki palepale wanaangalia maslahi na klabu ambayo inaweza kumkuza zaidi kiuchezaji mchezaji huyo ambaye malengo yake ni kufika mbali na kuisaidi afamilia yake kupitia soka.

“Kelvin ana kipaji kikubwa na anahitaji kufika mbali hatutaki kumpoteza kikubwa ni kuhakikisha tunamtafutia timu ambayo itatimiza malengo yake hatutamwangusha katika hili tutapambana kuona anafikia mafanikio,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply