Sunday, August 25

Kagere, Okwi, Bocco waipoteza Yanga nzima

0


By MWANDISHI WETU

MASHABIKI wa Yanga waliikejeli sana Simba walipowasajili, mastarika Emmanuel Okwi, John Bocco na Meddie Kagere wakiwaita vibabu a.k.a Wahenga, lakini kwa sasa hawana hamu nao kwa jinsi nyota hao wanavyofanya mambo makubwa Msimbazi msimu huu.

Bocco na Okwi walisajiliwa na Simba msimu uliopita na kusababisha klabu hiyo ichekwe sana na mashabiki wa Yanga na hata alipotua Kagere msimu huu akitokea Gor Mahia, mashabiki hao wa Jangwani waliendelea kuimba wimbo ule ule kwamba watani zao wamesajili babu.
Hata hivyo mpaka sasa nyota hao watatu wamefunga zaidi ya nusu ya mabao ya Yanga ambayo yamefungwa na wachezaji wao 13.
Naam, Kagere ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara kwa sasa ameifungia Simba mabao 16 kati ya 50 yaliyotiwa kambani kupitia mechi 23 iliyochezwa watetezi hao wa ligi hiyo.
Bocco ali yesajiliwa kutoka Azam FC, yeye ametupia kambani mabao 11, huku Okwi naye akifunga 7, ambapo uklichanganya mabao ya nyota hao watatu uitapata 34 ambayo ni zaidi ya nusu ya mabao 51 ya Yanga yaliyofungwa na wachezaji 13 kupitia mechi 32 ilizocheza mabingwa haop wa kihistoria.
Katika mabao hayo 51 ya Yanga, Heritier Makambo ndiye anaoongoza kwa kufunga mabao 15, huku mkongwe Amissi Tambwe akifuatiwa akiwa na mabao nane kisha Nahodha Ibrahim Ajibu aliyecheka na nyavu mara sita mpaka sasa.
Ukiichukua safu nzima ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Makambo, Ajibu, Tambwe na Mrisho Ngassa bado haiwezi kufikia mabao ya Kagere, Okwi na Bocco. Ngassa anmeifungua Yanga mabao manne sawa na kiungo Feisal Salum.
Na kama utaamua kuyaunganisha mabao ya kina Okwi, Kagere na Bocco sambamba na yale ya Adam Salamba aliyetupia kambani manne maana yake, idadi ya mabao ya safu ya ushambuliaji ya Simba itaipoteza kabisa ile ya Yanga kwani wakali hao watafikisha mabao 38 dhidi ya 33 tu.
Hata kama utaamua kuyajumuisha mabao 33 ya safu ya ushambuliaji ya Yanga sambamba na Deus Kaseke aliyefunga mawili, bado idadi hiyo haiwezi kufikiwa kwani itazidiwa matano.
Kagere aliyeifungia  Simba mabao sita katika Ligi ya Mabingwa Afrika aliwahi kukariri na Mwanaspoti kuwa, amekuja Tanzania kufunga mabao na sio kuuza sura na anafurahia anachotupia kila akipata nafasi na kudai ishu kwake sio kiatu cha Dhahabu bali kuisaidia timu yake.
“Mimi ni mshambuliaji, kazi yangu kufunga, nikifunga ni sehemu ya majukumu na nimekuja Simba ili kuipa mataji na kusaidia kupata mafanikio, nafurahia kuwepo hapa,” Kagere alinukuliwa.
Kwa taarifa yako tu mabao 50 ya Simba yamefungwa na wachezaji 9 wa klabu hiyo yakiwamo matatu ya Shiza Kichuya anayecheza soka la kulipwa nchini Misri, huku moja wakipewa ofa baada ya beki Erick Murilo kujifunga wakati akiichezea Stand United.
Wafungaji wengine wa mabao ya Simba ukiwaondoa kina Okwi, Kagere, Bocco na Salamba na Clatoyus Chama (4), Shiza Kichuya (3), Asante Kwasi, Mzamiru Yassin, Paul Bukaba na Said Ndemla kila mmoja akitupia moja.
Kwa upande wa Yanga wachezaji 13 wamehusika na mabao 51 wakiongozwa na Makambo mwenye mabao 15.
Wengine ni Tambwe  (8), Ajibu (6), Ngassa na Fei Toto (4), Rafael Daud, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Deus Kaseke na Papy Kabamba Tshishimbi ambapo kila mmoja amefunga mabao mawili, huku mabeki Kelvin Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’, kila mmoja amefunga bao moja moja sana na viungo Jaffar Mohammed na Thabani Kamusoko.

Share.

About Author

Leave A Reply