Tuesday, August 20

Kagere, Makambo hawashikiki

0


By MWANDISHI WETU

 KWA namna wanavyokimbizana Meddie Kagere na Heritier Makambo katika kuzifumania nyavu, kumewaibua hadi mafundi wa mpira, Emmanuel Gabriel na Boniface Pawasa, ambao wamesema kiatu cha dhahabu mbona kina moto.

Pawasa na Gabriel ambao waliichezea Simba na Taifa Stars miaka ya nyuma wamevutiwa na ushindani wa Makambo (Yanga) na Kagere (Simba) wakisema kuwa, wanajitambua na wanawajibika vilivyo kazini. Kwa sasa Kagere anaongoza kwenye msimamo akiwa na mabao 16 sambamba na Aiyee huku Makambo akiwafukuzia akiwa na mabao 15.

Pawasa alisema wanachofanya wachezaji hao kinatakiwa kiwafunze wazawa akidai wasiwe wasindikizaji kwenye timu hasa Simba na Yanga.

“Timu ambazo zinamhitaji Kagere ni kwa sababu ya kiwango chake na Simba ina nafasi kubwa ya kumtangaza kimataifa na hata kama atabaki basi dau lake litakuwa kubwa.

“Ukweli ni kuwa Makambo na Kagere wanaweza kunasa dili nyingi za kukipiga nje ya Tanzania, wanaifanya kazi yao vizuri na kila mmoja ana nafasi ya kuwa mfungaji bora ingawa kimahesabu Simba wana mechi nyingi tofauti na Yanga,” alisema Pawasa.

Naye Gabriel, alidai Makambo na Kagere wanajua thamani ya nafasi wanazocheza na fursa ambazo zipo ndani ya Simba na Yanga.

Alisema kwa jinsi wanavyotupia mabao kwa nyakati tofauti kulingana na majukumu ya timu hizo kwamba, kunaleta umakini na ushindani.

“Wivu wa maendeleo ndiyo huo unafanywa na Makambo na Kagere, kila mmoja anakuwa anasikilizia mwenzake anamiliki mabao mangapi basi anaongeza mzuka, lakini pia Salumu Aiyee amekuwa akipambana vya kutosha,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply