Wednesday, August 21

Kagere atoboa siri ya kiatu cha dhahabu

0


By Imani Makongoro

Dar es Salaam.Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2018/2019, Meddie Kagere wa Simba ametoboa siri ya kutwaa tuzo hiyo.

Kagere amepachika mabao 23 katika Ligi Kuu na kuisaidia Simba kutetea ubingwa msimu huu alisema siri ya tuzo hiyo ni kuzichukulia mechi zote za Ligi kwa uzito.

Alisema katika mechi zote alizocheza katika Ligi, hakuwahi kudharau mechi, kila moja aliipa uzito sawa.

“Nilikuwa nikipambana katika kila mechi, sikuwa na mechi kubwa wala ndogo, zote kwangu zilikuwa na uzito sawa,” alisema Kagere mara baada ya mechi yao ya mwisho ya Ligi na Mtibwa Sugar iliyokwisha kwa sare ya 0-0.

Alisema kila mechi aliipa uzito sawa na alijituma ili kuhakikisha anafanya vizuri na kuisaidia timu yake kuchukua pointi tatu.

“Kwangu kila mechi ilikuwa fainali, nashukuru Wana Simba wote, wachezaji kwa ushirikiano ulioniwezesha kutwaa tuzo hii, nitaendelea kujituma zaidi ili kuweka rekodi kwenye Ligi,” alisema Kagere.Share.

About Author

Leave A Reply