Thursday, July 18

Kaduguda: siogopi kuuliza haki hata kidogo

0


By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Mgombea ujumbe wa Simba, Mwina Kaduguda amesema, haogopi kuzungumza au kuuliza haki.
Kaduguda ambaye alizua hali ya sintofahamu wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Simba kwa sababu ya idadi ya watu kuongezeka kwa wingi ndani ya muda mchache.
Amesema, alifanya maamuzi na kuzungumza wazi kwa sababu ilikuwa haki yake.
“Tulifanya makubaliano na tukasaini kwa sababu ya jambo hilo, ndiyo maana sikuliacha nikazungumza,”alisema Kaduguda.
Kabla ya zoezi upigaji kura Kaduguda aliingilia zoezi la uchaguzi ambalo lilichafua hali ya hewa ka muda lakini baadaye walizungumza yakaisha.
Mgombea huyo aliyewahi ushika nyazifa za uongozi ndani ya Simba katika vipindi tofauti.
Alisema idadi ya kwanza ya wajumbe 1486, ikatajwa ya 1720, na mwisho 1728, ilikuwa ikiongezeka kwa wingi ndani ya muda mchache.

Share.

About Author

Leave A Reply