Thursday, February 21

Kabudi: Tuna kesi 13 za madai nje

0


By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Tanzania inakabiliwa na kesi za madai ya jumla ya Dola za Marekani 185,580,009.76 (zaidi ya Sh400 bilioni) kutoka na mashauri mbalimbali kwenye mahakama za kimataifa.

Hata hivyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi licha ya gharama hiyo inayotokana na mashauri 13 yaliyofunguliwa, hakuna shauri lililotolewa uamuzi hivyo sio madeni.

Waziri Kabudi alitoa kauli hiyo bungeni jana Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) ambaye pia alitaka kujua Serikali imejifunza nini kutokana na kesi hizo.

Katika swali lake, Zitto alisema Tanzania inakabiliwa na mashauri mbalimbali kwenye mahakama za kimataifa kama ya ICSID, ICA London na ICC Paris kuhusu masuala ya uwekezaji, “Kuanzia Novemba, 2015 mashauri hayo ni mangapi kwa idadi na yapo kwenye mahakama zipi na jumla ya madai yote ni kiasi gani.

Akijibu Waziri Kabudi alisema mashauri yaliyofunguliwa kuanzia Novemba 2015 ni 13 katika mahakama mbalimbali zikiwamo Permanent Court of Arbitration (PCA), London Court of International Arbitration (LCIA) na International Centre for Settlement of Investment Dispute (ICSID) na huko Johannesburg Afrika Kusini kupitia Sekretarieti ya UNICTRAL.

Alisema hakuna kesi iliyofunguliwa na kampuni ya Acacia Mining PLC na kwamba shauri namba Arbitration UN 173686 na Shauri UN 1736867, yamefunguliwa Julai 3 na kampuni ya Pangea Minerals Ltd na Bulyanhulu Gold Mining Ltd mtawalia.

Share.

About Author

Leave A Reply