Tuesday, March 19

JKU yachezea mbili safi yaaga Ligi ya Mabingwa

0


By Haji Mtumwa

Zanzibar. Mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, JKU imekubali kupigo cha mabao 2-0 kutoka kwa AL Hilal ya Sudan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kwa matokeo hayo JKU imeaga mashindano kwa jumla ya mabao 6-1 na kuungana na Zimamoto kuyaaga mashindano Afrika kwa msimu huu.

Katika mchezo huo JKU ilianza vizuri kwa kujilinda katika kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa hawajafungana.

Mambo yalibadilika katika kipindi cha pili kwa Al Hilal ilibadilika na kuanza kulisakama kwa nguvu lango la JKU kwa dakika zote.

Katika dakika ya 80, Sharaf Eldin Shiboub alifungia Hilal bao la kuongoza kabla ya Geovane Dinis kumalizia bao la pili katika dakika za nyongeza.

Kocha wa JKU, Omar Khamis aliwaomba radhi wapenzi na mashabiki baada ya kufanya vibaya katika mashindano hayo

Share.

About Author

Leave A Reply