Tuesday, March 19

Jinsi Rais Bush alivyompatia pipi mke wa Obama kanisani

0


By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Marekani. Utakuwa umekosea sana kama utashangazwa na kitendo cha Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kumpatia ‘pipi’ Michelle, mke wa rais mstaafu wa nchi hiyo,  Barack Obama.

Bush amefanya kitendo hicho katika ibada ya mazishi ya baba yake, George H.W Bush ambaye pia ni Rais mstaafu wa Taifa hilo.

Septemba, 2018 Bush alifanya tukio kama hilo baada  ya kumpa ‘pipi’ Michelle wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha Seneta wa Jimbo la Arizona, John McCain.

Leo Alhamisi Desemba 6, 2018 amerudia tena  baada ya video mbalimbali kumnasa Bush wakati akiwasili kwenye moja ya Kanisa maarufu la National Cathedral lililopo Jimbo la Washngton ambapo ibada ya mazishi ilikuwa ikifanyika.

Wakati anawasili kanisani hapo Rais huyo mstaafu aliingiza mkono wake wa kushoto mfukoni na kutoa Pipi hiyo ambayo baadaye alimkabidhi Michelle wakati wakisalimiana kwa kupeana mikono.

Wakati akiwa ameshikilia pipi hiyo, Bush alipeana  mikono na Obama na baadaye mkewe Michelle na kupatia kitu kinacholezwa kuwa ni pipi.

Baada ya kufanya hivyo, aliendelea kusalimiana na marais wastaafu wa nchi hiyo, Bill Clinton, Jimmy Carter na mkewe Rosalynn kabla ya kuketi kwaajili ya ibada hiyo iliyohuduriwa na viongozi wa juu wa Taifa hilo.

Kitendo hicho kimemfurahisha ,Michelle ambaye amesema kunatokana na ukaribu.

“Tuko pamoja muda wote, na ninampenda kupindukia, ni mtu wa aina yake na mcheshi,” amesema Michelle.

Baba yake Bush alifariki dunia Ijumaa Novemba 30, 2018 akiwa na umri wa miaka 94.

Share.

About Author

Leave A Reply