Monday, August 26

Japan kununua ndege 105 za kivita kutoka Marekani

0


Washington, Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump amesema Japan inamepanga kununua ndege 105 za kivita zilizotengenezwa nchi kwake.

Trump ambaye yuko nchini Japan kwa ziara ya kiserikali amesema nchi hiyo imetangaza nia yake ya kununua ndege mpya chapa F35 stealth.

Mwezi Desemba, Serikali ya Japan ilitangaza kuwa katika bajeti yake ya sasa ya ulinzi, inakusudia kununua ndege 105 chapa F35A, ambazo zinapaa na kutua kawaida.

Vyombo vya habari vya Japan viliripoti kwamba mauzo hayo huenda yakawa na thamani ya zaidi ya Yen trilioni moja ambazo ni sawa na Dola bilioni moja.

Katika hatua nyingine, Rais Trump amesema hatishwi na majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya masafa mafupi ya Korea Kaskazini na haamini kama yanakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Trump alitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi habari na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe wakati wa ziara hiyo.

Share.

About Author

Leave A Reply