Monday, March 18

Hii Yanga ni habari nyingine kabisa

0


Mbeya. Moto huu wa Yanga hakika haupimiki kutokana na kasi waliyonayo katika mechi zao za Ligi Kuu Bara na sasa inaendelea kutamba kileleni.

Iko hivi, mpaka sasa Yanga na Azam FC ndiyo timu pekee hazijafungwa, lakini upekee wao ni kwamba, kila wanapokwenda kucheza ugenini wanapiga tu.

Ushindi wao wa mabao 3-1, walioupata leo Jumatatu dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ni wa 12 kwa Yanga huku wakiwa wametoka sare mbili tu. 

Walioing’arisha Yanga katika mchezo huo ni Ibrahim Ajibu aliyefunga bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 76, likifungwa baada ya Jumanne Elfadhili kuifungia Mbeya City bao la kuongoza ambalo pia ni la mkwaju wa penalti dakika ya 45.

Mkali wa mabao wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe ambaye sasa ni kama amerudi kwa kasi baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na maumivu ya mguu, ndiye aliyekazia ‘msumari wa moto’ kwa Tanzania Prisons akipachika bao la pili dakika ya 84 na  la tatu ndani ya dakika za nyongeza baada ya 90, kumalizika.

Katika mchezo huo kali zaidi ilikuwa ni vuta nikuvute za hapa na pale, beki wa Yanga Andrew Vincent ‘Dante’ alipewa kadi ya njano na mwamuzi Meshack Suda baada ya kuonyesha ishara ya utovu wa nidhamu kwa mwamuzi huyo.

Dante alionyesha ishara ya kugomea uamuzi yake na kama alitaka kumpiga kichwa.

Pia, Mrisho Ngassa alimpiga kichwa Hassan Kapalata na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Pia, nahodha wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile wa Tanzania Prisons kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyesha hali ya utovu wa nidhamu uwanjani.

Share.

About Author

Leave A Reply