Saturday, August 17

Hazard kuvuta Pauni 400,000 kwa wiki Madrid

0


REAL Madrid imemuahidi staa wa Chelsea, Eden Hazard, 28, mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi kwa ajili ya kuhakikisha staa huyo anatua Santiago Bernabeu katika dirisha kubwa lijalo la Usajili.

Inaeleweka tayari Hazard amekutana na wawakilishi wa Real Madrid kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa kwenda Hispania ambapo Madrid wanatarajia kulipa kiasi cha Pauni 100 milioni kwa staa huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji.

Hazard ameamua kuondoka Chelsea baada ya kugoma kusaini ofa tatu za mkataba klabuni hapo na Madrid inamuona kama mbadala wa muda mrefu wa staa wao wa zamani, Cristiano Ronaldo ambaye msimu huu ilishindwa kuziba pengo lake.

Mabosi wa Chelsea nao wanaonekana kushindwa kumwachia nyota huyo kutokana na adhabu wanayoitumikia kwa sasa ya kutosajili na wanatumia mwanya huo kuwashawishi baadhi ya mastaa kubaki klabuni hapo.

Share.

About Author

Leave A Reply