Saturday, August 24

Hazard ataja tarehe ya kutua Real Madrid

0


LONDON, ENGLAND. HABARI ndiyo hiyo. Eden Hazard anataka dili lake la kujiunga na Real Madrid likamilike katika muda usiozidi wiki moja baada ya fainali ya Europa League.
Staa huyo wa Chelsea ameweka tarehe ya mwisho wa kuhusu dili hilo kwamba hadi Juni 4 liwe limekamilika, huku Real Madrid wakizidi kuchochea mpango wao wa kunasa huduma ya Mbelgiji huyo kwa nguvu zote.
Hata hivyo, Real Madrid kwenye ofa yao kuna upungufu wa Pauni 26 milioni kutoka kiwango kile ambacho Chelsea wanataka walipwe kwenye mauzo ya mchezaji huyo. Los Blancos wao wamewekwa mezani ofa ya Pauni 86, lakini Chelsea wanataka Pauni 112 milioni.
Makubaliano yanatarajiwa kufikiwa ili kutimiza ndoto za mchezaji huyo ambaye amepania kwa nguvu zote kuhama Stamford Bridge na kutua Santiago Bernabeu.
Na kinachoelezwa ni kwamba ameshawaambia marafiki zake kuhusu dili kukamilika kabla hajaenda kujiunga na timu yake ya taifa ya Ubelfiji kwa ajili ya mechi ya kufuzu Euro 2020 dhidi ya Kazakhstan, Juni 8 na ile ya Scotland, Juni 11.
Kocha wa zamani wa Hazard huko Chelsea, Jose Mourinho alisema anachokiona uhamisho huo unaenda kutokea, akisema: “Inavyoonekana kabisa Hazard anacheza mechi zake za mwisho Chelsea. Ni mchezaji aliyekuwa muhimu sana Chelsea katika kizazi cha karibuni. Lakini, anataka kushinda na hilo ndilo linamfanya aende Real Madrid.”


Share.

About Author

Leave A Reply