Friday, August 23

Gwajima: Ni muhimu kujitegemea

0


Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephati Gwajima amewataka watu kujifunza kujitegemea.

Aliyasema hayo leo Aprili 21 wakati akitoa somo katika misa  ya sikukuu ya Pasaka na kuongeza kuwa kuna binadamu wengine wapo kwaajili ya kuwachelewesha wenzao ili maisha yawe magumu.

 “Kuna wakati unaona mambo hayaendi umekwisha kata tamaa jifunze kujipambania.” Alisema Gwajima

Gwajima amesema ukame unafaidi kwa kuwa unaifanya mizizi ya  miti kutambaa kwenda chini zaidi kutafuta maji ili mti huo usife lakini kunapotokea upepo pia hauwezi kung’oka.

Amebainisha kuwa Mkristo asiyezoea kujitegemea panapotokea jambo utamkuta amekwisha hamia katika nyumba ya jirani kwa sababu hakuachwa aweze kujitegemea ili kutafuta kuishi.

Hivyo aliwataka watu kuanza sasa kujifunza  kujitegemea na kwamba hakuna jambo zuri kama kuwa  na mtu wa kukuongoza, “huwezi jua umuhimu wake hadi siku utakapo mpoteza”.

Amesema kuna binadamu wapo kwa ajili ya kuharibu na kupindisha njia za maisha ya wenzao na kuwachelewesha kufikia malengo.

Share.

About Author

Leave A Reply