Tuesday, August 20

Four Ways bingwa bonanza la Castle Africa 5 aside

0


By Majuto Omary

Dar es Salaam.Timu ya Four Ways Park Fc imetawazwa kuwa bingwa mpya kwenye bonanza la Castle Africa 5 aside lililofanyika Leo Aprili 28 jijini Dar es Salaam.

Katika bonanza hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager lililofanyika kwenye Viwanja vya Posta Kijitonyama mabingwa hao walizibwaga timu nyingine 32.

Ushindi huo, timu ya Four Ways ilizawadiwa kombe, Medali za dhahabu, Pesa taslimu Sh1.5 Milioni, Caton ya bia za Castle Lager pamoja na kupata fursa ya kuwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini.

Katika matokeo ya jumla, Four Ways Park Fc waliutwaa ubingwa kwa pointi 7 wakifuatiwa na Jacks Pub Fc iliyopata pointi nne na kushinda medali za fedha, katoni ya bia za Castle Lager na pesa taslimu Sh 900,000.

Meeda Night Club Fc ambao walipata pointi 3 waliibuka na medali za shabak walizawadiwa pia katoni ya bia za Castle Lager pamoja na fedha Sh 600,000.

Meneja wa bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alizipongeza timu hizo kwa ushindi na kuwasisitiza mashindano hayo yawe chachu kuelekea kwenye yale ya Afrika Castle 5s yatakayofanyika nchini.

Pamela aliutaja mchakato ulivyokuwa wa kuzipata timu ulianzia katika Baa 60 za jijini Dar es Salaam ambapo Bar zilishindana kwa kununua Bia za Castle Lager na kukusanya vizibo na mwisho tukapata timu 32 zilizoongoza na ndizo zimeweza kushiriki Bonanza mpaka kumpata Bingwa ambaye ni Four Ways Park Fc.

Balozi wa Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda aliishukuru TBL kwa uratibu mzuri wa mashindano ya Castle Africa 5s mwaka huu kwani yamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuwaomba waendelee kudhamini mashindano hayo.

Share.

About Author

Leave A Reply