Friday, April 19

Eti! Hazard anatafuta nyumba huko Madrid

0


MADRID, HISPANIA . SUPASTAA, Eden Hazard ameripotiwa kuanza mchakato wa kutafuta makazi huko Madrid ikiwa ni mwanzo tu wa kutimiza malengo yake ya kwenda kujiunga na Real Madrid.

Kumekuwa na ripoti Hazard kwa sasa mipango yake ni kwenda kujiunga na Real Madrid na hilo linaaminika linaweza kutokea mwishoni mwa msimu huu.

Mchambuzi mmoja maarufu wa soka huko Hispania, Eduardo Inda, alifichua Hazard ameanza kutafuta nyumba ya kuishi huko La Finca.

“Hazard ameshaanza kutafuta nyumba ya kuishi Madrid na (Thibaut) Courtois anamsaidia kufanya hivyo. Wao ni marafiki wakubwa wa karibu sana,” alisema Inda.

“Wamempa kazi dalali mmoja wa majumba kuomba wanapata wapi. Anachotaka ni kuishi La Finca, naona kabisa atanunua nyumba. Kitu kingine anaweza kuifikia pia nyumba anayoishi Gareth Bale kwa sababu inavyoonekana ataondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu. Nyumba ya Bale ina historia, Hazard atakuwa staa wa tatu mkubwa kuishi hapo, huko nyuma alikuwa Kaka.”

Share.

About Author

Leave A Reply