Sunday, August 25

Duh! Van Dijk naye Madrid wanamtaka

0


MADRID, HISPANIA.UTASIKIA mengi sana kipindi hiki. Jingine linalosemwa kwa sasa ni kwamba Real Madrid wameamua kumweka kwenye mipango yao beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk aje kwenye kikosi chao kama Sergio Ramos ataamua kuondoka Bernabeu.

Katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya kumekuwa na mambo mengi ikiwamo ya Ramos kuhusishwa na mpango wa kuachana na Real Madrid, akidaiwa kutibuana na rais wa timu hiyo, Florentino Perez.

Liverpool na Manchester United zilitajwa kwamba zinamtaka nahodha huyo wa Los Blancos, lakini taarifa za karibuni Liverpool wamekanusha kuwa na mpango wa kumchukua Ramos, ambaye amekuwa hana uhusiano mzuri na supastaa wa Anfield, Mohamed Salah.

Kwa mujibu wa AS, staa Ramos akiondoka Bernabeu, basi Real Madrid watafanya kila wanaloweza kumnasa Van Dijk, ambaye ni mmoja wa mabeki bora kabisa wa kati duniani kwa sasa.

Hata hivyo, jambo hilo halitakuwa kirahisi kihivyo kwa sababu Liverpool hawatakuwa tayari kuuza mchezaji wao muhimu kiasi hicho, tena kumuuza kwa wapinzani atakaochuana nao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Beki Van Dijk amefunga mabao sita na kuasisti mara nne katika mechi 49 alizoichezea Liverpool ya kocha Jurgen Klopp msimu huu.Share.

About Author

Leave A Reply