Saturday, August 24

Dk Kigwangalla agoma kulipunguza pori la akiba la Maswa

0


By Mussa Juma, Mwananchi [email protected]

Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema pori la akiba la Maswa halitapunguzwa kwa maelezo kuwa limebainika kuwa makazi ya Faru.

Akizungumza leo Jumamosi Mei 18, 2019 katika zoezi la ufungaji mikanda ya mawasiliano ya kijiografia (GPS) kwa Tembo 18 waliopo katika pori hilo na hifadhi ya jamii ya Makao, Kigwangalla amesema pori hilo litaendelea kuhifadhiwa.

“Kulikuwa na maombi kupitia mbunge aliyetaka tulipunguze tena pori la akiba ya Maswa, lakini kutokana na ushauri wa kitaalam na kubainika sasa Faru wanatoka Serengeti na kuja katika eneo hili la asili hatutalipunguza tena, “ amesema.

Amebainisha kuwa  Pori la akiba la Maswa linalopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, hadi sasa kuna maeneo yamevamia na kulifanya kuwa dogo.

“Hatuwezi kuendelea kulipunguza eneo hili kwani imedhihirika ni eneo la asili za Faru, sasa wanaishi wakitoka eneo la Serengeti,” amesema.

Akizungumzia pori hilo mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema ni muhimu  kwa mustakabali wa uhifadhi nchini kwani pia ndio sehemu ambayo nyumbu wa Hifadhi ya Serengeti huenda kuzaa watoto.

Share.

About Author

Leave A Reply