Tuesday, July 23

Diwani Chadema atuhumiwa kusababisha biashara ya ukahaba, akana

0


Dar es Salaam. Wakazi wa kata ya Kijitonyama wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamemtupia lawama diwani wa kata hiyo, Juma Uloleulole (Chadema) wakidai anasababisha biashara ya ukahaba kuendelea katika kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo jioni, mmoja wa wakazi hao alimtaja Uloleulole akidai ana ratibu biashara hiyo na kuyafahamu madanguro.

“Huyu diwani ni mbabaifu, kuna uwezekano anakatiwa kitu huyu maana haiwezekani madanguro anayajua halafu anayafumbia macho,” alisema.

Akijibu tuhuma hizo, Uloleulole alisema madai hayo hayana ukweli na yana lengo la kumchafua kisiasa.

Uloleulole ambaye ni diwani kwa tiketi ya Chadema alidai tuhuma hizo zinatolewa na mahasimu wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Hayo mambo hayapo ni mahasimu zangu wanataka kunichafua ila mie nawaambia hawatafanikiwa na uchaguzi ujao nawapiga tena,” alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply