Friday, May 24

Dengue bila bima utalipia matibabu

0


By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali haijatoa majibu kuhusu matibabu kwa wagonjwa wa dengue kama watatibiwa bure au kwa gharama badala yake wamesema watu wenye bima wataendelea kutibiwa bure katika vituo vya umma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Faustin Ndugulile ameliambia Bunge leo Ijumaa Mei 17, 2019 kwamba Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika swali la nyongeza mbunge wa Ulanga (CCM)  Goodluck Mlinga ameuliza ni kwa nini Serikali isitoe matibabu bure kwa wagonjwa wa dengue.

Naibu Waziri amesema hadi wiki hii kulikuwa na wagonjwa 1,901 katika mikoa ya Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Singida na Dar es Salaam ambapo tayari wameshapata vipimo ambavyo vilikuwa havipo.

Katika swali la msingi mbunge wa viti maalum (CCM) Mwantumu Dau Haji alitaka kujua Serikali ina mkakati gani katika kuwashughulikia ipasavyo wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na kansa.

Dk Ndugulile amesema magonjwa yasiyoambukiza yana gharama kubwa katika matibabu yake hivyo Serikali imeamua kupeleka bungeni muswada wa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya ili kupunguza makali ya gharama.

Ametolea mfano wa kupandikizwa figo ni Sh20 milioni wakati gharama za kusafisha damu kwa mgonjwa ni Sh 750,000 hadi 1 milioni kwa wiki ambayo ni gharama kubwa.

Share.

About Author

Leave A Reply