Sunday, August 18

Dante: Hali ya hewa Moro inatupa mzuka

0


Beki wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ amesema hali ya hewa  Morogoro inawasaidia kufanya mazoezi bila kuchoka kujiandaa na mechi yao Kombe la FA dhidi ya Singida United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Dante alisema mechi hiyo wanaichukulia kama fainali, ili waweze kusonga mbele, akisisitiza kwamba ndio maana maandalizi yake ni mazito.

“Singida si timu ya kubeza ina wachezaji wenye ushindani wa juu, ndio maana tunajiandaa kikamilifu ili kukabiliana nao, lengo ni kutinga nusu fainali ya mashindano hayo,” alisema Dante.

Winga wa Singida United, Deus Kaseke alisema wanaiheshimu Yanga, lakini sikuiogopa uwanjani, hivyo wanajipanga kukabiliana nao, kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

“Nimeichezea Yanga, naijua si timu ya kuibeza hata kidogo, uzuri hata kocha anaielewa vizuri, hatuwezi kupuuza mechi hiyo kwani inaweza kutufanya tukasonga mbele kwenye Kombe la FA na mwisho wa siku tukachukua ubingwa,” alisema Kaseke.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.