Tuesday, August 20

Damu mpya inavyowakimbiza wakongwe kwenye dansi

0


By Rhobi Chacha Mwananchi

MUZIKI wa dansi kwa sasa ni kama unajikongoja. Ikiwa bado muziki huu unajikongoja, kumeibuka wasanii wachanga au tuwaite damu mpya na wanafanya vizuri na ujio wao umekuwa chachu katika harakati za kuusimamisha tena muziki huo.

Kazi za damu mpya zimejizolea umaarufu kwa sasa na kuzoa mashabiki wengi kila kona,tofauti na za wakongwe ambao wameadimika katika chati za muziki huo. Hawa ni baadhi ya wanamuziki damu changa ambayo mwaka huu inawakimbiza wakongwe.

Jina lake halisi ni Almasi Djuma. Miezi nane iliyopita alitoa wimbo ‘Coco Channel’ uliomtambulisha kwa wadau wa muziki wa dansi na kupewa jina la Mfalme wa Rhumba kutokana na wimbo huo kuwashika mashabiki wake. Staa huyu wiki chache zilizopita ameachia wimbo mwingine ‘Chozi Langu’ ambao kwa sasa uko vema kwenye ulimwengu wa muziki wa dansi.

Jimmy Manzaka ambaye malengo yake kimuziki anataka apige muziki wa kimataifa kama kina Fally Ipupa, Ferre gola, Heritier Watanabe na wengine, amesema kutokana na kufanya kazi kama mwanamuziki binafsi hivyo ana mpango wa kufanya shoo pindi atakapofikisha nyimbo nne sababu anataka akiwa jukwaani awaburudishe wadau wa muziki wa dansi nyimbo zake kama zake na sio kopi kama wanavyofanya wanamuziki wengine.

Huyu ni mwanamuziki mwenye historia ya kupitia bendi nyingi ikiwamo Utalii, Twanga Academia, African Beats na nyinginezo ,ila aliamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea baada ya kuona ana uwezo wa kujisimamia mwenyewe.

Wimbo uliomtambulisha toka alipoanza kuimba binafsi ni Papaa Fololo, ‘Nikoleze na Bye zinazoendelea kufanya vizuri kitaani.

Wiki mbili zilizopita ameachia wimbo mpya ‘Upepo’amemshirikisha mwanamuziki Papii Kocha.

Anasema sababu ya kumshirikisha Papii Kocha katika wimbo wa Upepo ni “Papii kocha wakati ametoka tu jela, alisikika mara kwa mara akinitaja kwamba ni kati ya wanamuziki ambao alikuwa anawasikiliza sana wakati yupo gerezani na wimbo aliokuwa anaupenda sana ni wa ‘Nikukoleze’.

Malengo yake katika muziki wa dansi ni kuacha alama kwenye muziki kimataifa na kuyaenzi yote waliyowaachia wanamuziki wakubwa wa zamani, kuyaendeleza na kuenzi utamaduni asili wa muziki halisi kwenye majukwaa ya kimataifa na kubaki na utambulisho wake wa kipekee wa Kitanzania.

Ni mwanamuziki wa bendi ya Bogoss Musica iliyo chini ya Nyoshi El Saadat. Mbali na kuwa katika bendi hiyo pia anatoa nyimbo nje ya bendi kutokana na ruhusa ya kiongozi wa bendi hiyo.

Kelly Haso ambaye jina lake halisi ni Ally Said takribani miezi miwili iliyopita aliachia wimbo wake ‘Comeback’ na wiki moja iliyopita ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Nashindwa’ ambao ni rhumba. Anasema malengo yake ni kuufikisha nje ya Tanzania muziki wake na kufanya shoo kwa ajili ya kujitangaza kama msanii. Aidha Kelly Haso amezungumzia suala linalodaiwa na baadhi ya wadau kuwa wanawakimbiza katika muziki huu kwa sasa ambapo amesema: ”Kutokana na mfumo tu ukiwa binafsi kutoa nyimbo unaamua mwenyewe ila kwenye bendi mpaka uongozi ukae uamue nyimbo ipi itoke na kwa wakati gani.”

Ni mwanamuziki ambaye hapo mwanzo alianza kuimba nyimbo za Bongo Fleva lakini alipoona hapati mapokezi mazuri ndipo alipogeukia muziki wa dansi na kutoa wimbo wake ulioitwa “Movie”. Ni rhumba ambayo imepata mapokezi mazuri kwa wadau wa muziki wa dansi.

”Kwa sababu hiki ni kizazi kipya, naamini wakongwe pale walipofanya wao pametosha, sisi tunakuja kuanzia pale walipofikia wao na kuliendeleza gurudumu kwa maana muziki hauna mwenyewe.”

Share.

About Author

Leave A Reply