Sunday, August 25

Chelsea yaishusha Arsenal England

0


London, England. Chelsea imepanda hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England licha ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Chelsea imeishusha Arsenal katika nafasi hiyo baada ya kutoka sare hiyo dhidi ya  Burnley kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Wapinzani wake Tottenham Hotspurs, Arsenal na Manchester United ziliteleza kwa kufungwa katika mechi zao za mwishoni mwa wiki.

Mabao yote manne katika mchezo huo yalipatikana dakika 24 za kipindi cha kwanza.

Mchezaji Jeff Hendrick alianza kuifungia Burnley dakika ya nane kabla ya N’Golo Kante kusawazisha dakika ya 12.

Mshambuliaji nguli Gonzalo Higuain alifunga bao la pili dakika ya 14 kabla ya Ashley Barnes kusawazisha dakika ya 24.

Burnley imebaki katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kuziacha Cardiff,  Fulham na Haddersfield zikipambana na janga la kujinasua kuteremka daraja.

Share.

About Author

Leave A Reply