Monday, March 18

Burundi yaishutumu Rwanda

0


Bujumbura, Burundi. Rais Pierre Nkuruziza ameziomba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuandaa kikao maalum kwa ajili ya kujadili kile alichoelezea kuwa ni “mgogoro wa wazi” uliopo na jirani yake Rwanda.

Katika barua iliyosambazwa kwanza kwenye mitandao ya kijamii na baadaye vyanzo vya habari kutoka ikulu kulithibitishia shirika la habari la AFP, Rais Nkuruziza ameishutumu Rwanda kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro ulioko ndani ya Burundi uliodumu tangu Aprili 2015.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania, Sudan Kusini na Burundi.

“Rwanda ndiyo nchi pekee katika ukanda huu iliyojitokeza kuwa mshirika wakuu katika kuvuruga uthabiti wa taifa langu na kwamba siichukulii tena kama taifa mshirika, bali kama adui wa nchi yangu,” ilisema sehemu ya barua hiyo, ambayo inaonesha ilitiwa saini na Rais Nkurunziza Desemba 4.

Barua hiyo ambayo ameandikiwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye ni mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, imesisitiza kwamba Rwanda ndiyo iliandaa na kuwaunga mkono wakimbizi wa Burundi waliotaka kulivuruga taifa hilo.

Mgogoro baina ya Burundi na Rwanda umeendelea kukua baada ya Rais Nkurunziza kusema kwa uwazi kwamba mwenzake wa Rwanda Paul Kagame alipanga kuing’oa serikali yake katika mapinduzi yaliyoshindwa ya Mei 13, 2015.

Katika barua hiyo, Nkurunziza amemwambia Museveni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa EAC, kwamba “mbali ya ukweli kwamba Rwanda iliandaa na kusimamia mapinduzi ya mwaka 2015, watu waliohusika na wahalifu wengine wameweka makao katika nchi wanayoungwa mkono kuishambulia Burundi; wakivuka mpaka wa Rwanda-Burundi au kupitia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikiwa ni pamoja na kuwapatia usaidizi na nyaraka za kusafiria kuwawezesha kuzunguka katika eneo hili na hata Ulaya.”

Inafahamika kwamba hii si mara ya kwanza katika miaka kadhaa Nkurunziza akizungumzia kile anachokiita “uvamizi wa Rwanda” katika barua alizowaandikia viongozi wa ukanda huu.

Lakini barua ya Ijumaa ilikuwa na maneno makali na nakala zake ziliztumwa kwa Kagame, Uhuru Kenyatta wa Kenya na kiongozi wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ambao wamesisitiza juu ya kukua kwa mgogoro wa usalama huku wanadiplomasia wakijitahidi kuupatia 

Share.

About Author

Leave A Reply