Thursday, August 22

Bunge lamchagua Ramaphosa Rais Afrika Kusini

0


Bunge la Afrika Kusini jana Jumatano lilimchagua tena Cyril Ramaphosa kuwa Rais, ikiwa ni wiki mbili baada ya chama tawala cha ANC kushinda uchaguzi wa Bunge.

“Ramaphosa amechaguliwa kuwa rais, baada ya kuteuliwa mgombea pekee wa nafasi hiyo,” Jaji Mkuu Mogoeng Mogoeng alilieleza Bunge jijini Cape Town.

Wabunge wa Chama cha tawala cha ANC kilichoshinda viti 230 Mei 8,  walimchagua raia huyo katika kikao cha kwanza cha Bunge la nchi hiyo lenye wabunge 400.

ANC ilishinda uchaguzi wa Bunge kwa asilimia 57.5 ya kura zote, ikiwa ni ushindi wake wa chini tangu kuimalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Ramaphosa aliyechukua uraia katikati mwa muhula uliopita baada ya Jacob Zuma kujiuzulu Februari 2018, ataapishwa Jumamosi na anatarajiwa kutangaza Makamu wa Rais na baraza lake la mawaziri mwishoni mwa wiki.

Share.

About Author

Leave A Reply