Thursday, July 18

Bunge la EALA kujadili bajeti ya 2019/20 ya Sh249.8 bilioni

0


By Filbert Rweyemamu, Mwananchi [email protected]

Arusha. Bunge la Afrika Mashariki (Eala) litajadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2019/2020 ya kiasi cha dola 109.8 milioni sawa na Sh 249.8 bilioni.

Bajeti hioyo ni ongezeko la asilimia 10 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 iliyokua dola 99.7 milioni sawa na Sh 226.9 bilioni.

Kikao cha Bunge hilo kimeanza leo Jumatatu Juni 17, 2019 huku hotuba ya bajeti ikitarajiwa kusomwa siku ya Jumatano na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Rwanda, Dk Richard Sezibera.

Fedha hizo ni michango ya kila mwaka kutoka nchi wanachama ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Sudani Kusini, Uganda na Tanzania  ambayo mmoja atatoa  dola 8.3 milioni sawa na Sh 18.8 bilioni pia wahisani wa maendeleo watachangia dola  52.8 milioni sawa na Sh 120.2 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.

Ofisa Habari Mwandamizi wa Eala, Bobi Odiko amesema maandalizi ya mkutano huo wa bajeti yamekamilika na wabunge wameshawasili jijini Arusha kwaajili ya mkutano huo.

Vyanzo vingine vya mapato ni kutoka wizara nyingine za nchi wanachama kiasi cha dola 6.4 milioni sawa na Sh 14.6 bilioni, Vyuo Vikuu vitachangia dola 468,300 sawa na Sh 1.065 bilioni ,mapato mengine ni dola 283,745 sawa na Sh 645.5 milioni na kiasi cha dola 7.2 milioni sawa na Sh 16.3 bilioni ni mapato yatakayoelekezwa moja kwa moja kwenye miradi.

Katika mgawanyo wa matumizi Sekretarieti ya EAC imetengewa  Sh117.9 bilioni kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na kiasi cha Sh103.6 bilioni ilizopata katika mwaka wa Fedha 2018/19,Mahakama ya Afrika Mashariki(EACJ) imetengewa Sh 9.3 bilioni wakati bunge la Eala limetengewa Sh 43 bilioni.

Bonde la Ziwa Victoria (LVB) limetengewa kiasi cha Sh 30 bilioni ,Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki(EASTECO) imetengewa Sh 4.3 bilioni na Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(EAKC) yenye makao yake Zanzibar imetengewa Sh 3 bilioni .

Share.

About Author

Leave A Reply