Tuesday, March 19

Bulaya amvutia pumzi Ndugai

0


By Ephrahim Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Ester Bulaya amesema licha ya kupongezwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuibua suala la kikokotoo kipya cha mafao ya kustaafu, anampa nafasi kuchukua hatua na iwapo hataridhishwa atawasilisha hoja bungeni kutaka marekebisho ya sheria.

Bulaya alisema alipokea pongezi kutoa kwa Ndugai baada ya kuibua suala la kikokotoo kipya cha mafao na ataendelea kulifuatilia kwa karibu, na iwapo hataridhishwa na hatua zinazochukulia atachukua hatua zaidi.

“Spika alinipongeza na kusema hajafurahishwa na utaratibu huo mpya wa mafao, tayari aliita kamati ya sheria ndogo ili kushughulikia suala hilo, ngoja kwanza nimwache afanye kazi yake na hiyo kamati lakini nisiporidhishwa nitapeleka hoja bungeni ya mabadiliko ya sheria,” alisema Bulaya.

Bulaya ambaye pia ni mbunge wa Chadema Jimbo la Bunda Mjini, alikuwa akizungumza na wanahabari jana huku akipendekeza mfumo wa mafao nchini uwe kama wa nchi ya Canada.

“Canada mtumishi anaamua mwenyewe kiasi cha mkupuo atachukua, iwe ni asilimia 100, 75 au 50 hapangiwi, lakini pia Ufaransa mifuko ya hifadhi ya jamii inasimamiwa na watumishi wenyewe siyo Serikali na hivyo ndivyo inavyotakiwa,” alisema.

Bulaya aliomba uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wote kwa kuwa utaratibu wa sasa unaleta utata mkubwa miongoni mwa watumishi na kwamba, Bunge lina mamlaka ya kuuondoa utata huo. Pia, alisema wabunge wa CCM sasa wanatakiwa kutumia wingi wao kuwatetea wafanyakazi.

Share.

About Author

Leave A Reply