Saturday, July 20

Bondia afariki baada ya kupigwa KO

0


Bangkok, Thailand. Bondia wa Italia, Christian Daghio, amefariki Dunia juzi wiki moja baada ya kupigwa KO na Don Pareuang wakiwania ubingwa wa Dunia wa WBC wa mchezo wa Muay Thai.

Daghio mwenye miaka 49 alifariki Dunia katika hospitali mjini Bangkok, Thailand wiki moja tangu alazwe baada ya kupigwa kwa KO raundi ya kumi na Pareuang.

Bondia huyo alidondoshwa ulingoni mara mbili, mara ya mwisho mwamuzi alilazimika kuwaita madaktari kumsaidia na ilibidia akimbizwe hospitali ambako alifariki wiki moja baadaye, akiacha mke na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.

Daghio aliyecheza mapambano 189 na kushinda 145 kati ya hayo alihamishia makazi yake nchini Thailand.

Share.

About Author

Leave A Reply