Tuesday, March 19

Biashara yatua Dar, Yanga kutua kesho

0


By THOMAS NG’ITU

Dar es Salaam. KLABU ya Biashara United imetia timu jijini na tayari imeanza mazoezi mepesi leo jioni kwaajili ya kuikabili Yanga Jumapili, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Biashara watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Yanga kutokana na wapinzani wao watakuwa hawapo tayari kukubali rekodi yao ya kutokufungwa kupotezwa kirahisi.

Pia Biashara United nao waliotoka kupoteza dhidi ya Lipuli kwa kipigo cha 2-1, hawatokuwa tayari kuona wimbi la kipigo likizidi kuongezeka katika kikosi chao.

Hata hivyo Biashara wakiwa wameshawasili jijini hapa, klabu ya Yanga nayo inatarajiwa kuingia kesho wakitokea mkoani Sumbawanga ambapo walikuwa wameenda baada ya kutoka mkoani Mbeya walipocheza na Tanzania Prison.

Share.

About Author

Leave A Reply