Saturday, August 24

Benki ya CBA yataja faida nyingi za Mfumo wa Bulk Mobile Payment

0


Bulk Mobile Payment  ni mfumo unaowawezesha wateja kufanya malipo ya mtu mmoja mmoja au ya watu wengi kwa wamiliki wa simu wenye huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao. Hii inahusisha waajiri wanaofanya malipo kwa wafanyakazi ambao hawapo katika mfumo rasmi wa ajira (vibarua), makampuni ya bima yanayofanya malipo kwa wateja wao wasio na akaunti za benki, utoaji wa mikopo kwa wateja wasio na akaunti za benki, makampuni ya usafirishaji yanayotoa posho na mishahara kwa wasafirishaji (madereva) nk.

Moja ya matamanio ya Benki Kuu ya Tanzania na Taasisi zote za Kifedha nchini ni kuona kunakuwa na idadi ndogo ya fedha mtaani hususani katika kipindi hiki ambacho ulimwengu unaendelea kuhama kutoka analojia na kwenda digitali.

Hali hii ya kuwepo kwa kiwango kidogo cha fedha kinachobebwa mkononi ni moja ya mkakati madhubuti wa kuweza kukabiliana na hatari ya kuibiwa, kutapeliwa, kushambuliwa na wahalifu kutokana na kubeba fedha nyingi.

Benki nyingi na taasisi nyingine za kifedha zimekuwa zikijitahidi kuendana na kusudi hilo kwa kuanzisha huduma mbalimbali za kufanya miamala ya kibenki kwa njia ya mtandao yaani (Mobile banking, Masterpass QR Code n.k.).

Katika kuendelea kuunga mkono lengo hilo, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imeanzisha mfumo wa Bulk Mobile Payment ambao umebuniwa ili kurahisisha malipo ya watu wengi kwa mkupuo na kuhakikisha usalama wa malipo hayo.

Meneja Maendeleo wa Benki ya CBA, Huduma za Kibenki za Makampuni na Uwekezaji, Ruth Kalonga anaelezea kwa kina kuhusiana na mfumo huo wa Bulk Mobile Payment.

Tuelezee kwa ufupi kuhusu Mfumo wa Bulk Mobile Payment

Huu ni mfumo unaowawezesha wateja kufanya malipo ya mtu mmoja mmoja au ya watu wengi kwa wamiliki wa simu wenye huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao. Hii inahusisha waajiri wanaofanya malipo kwa wafanyakazi ambao hawapo katika mfumo rasmi wa ajira (vibarua), makampuni ya bima yanayofanya malipo kwa wateja wao wasio na akaunti za benki, utoaji wa mikopo kwa wateja wasio na akaunti za benki, makampuni ya usafirishaji yanayotoa posho na mishahara kwa wasafirishaji (madereva) nk.

Malipo haya yote yanafanyika kupitia huduma za kibenki za CBA za mtandaoni za kisasa. Mteja anachotakiwa kufanya ni kuweka mtandaoni jalada/ orodha ya majina ya wanufaika, namba zao za simu na kiasi kinachohitajika kuhamishwa kwenda kwa mhusika.

Moja ya sifa ya bidhaa hii ni pamoja na kuwezesha zaidi ya watu 1000 kulipwa kwa wakati mmoja, malipo yanafanyika kwa haraka zaidi, mchakato wake ni rahisi ambapo kikubwa kinachofanyika fedha zinalipwa kwa kuhamishwa kutoka kwenye akaunti ya mteja na kwenda katika huduma za mitandao ya simu mbalimbali kama vile (Tigopesa, M-pesa, Airtel money nk).

Makampuni makubwa ambayo yanaendesha akaunti za benki mbalimbali lakini yanalazimika kufanya malipo ya fedha taslimu ambayo kimsingi ni hatari, yatagundua kuwa bidhaa kutoka Benki ya CBA wenye msaada wa kutumainiwa.

Zipi ni faida za mfumo wa Bulk Mobile Payment?

Moja ya faida zinazopatikana kutokana na matumizi ya mfumo huu wa Bulk Mobile Payment kufanya malipo ni kukabiliana na hatari inayoweza kumkumba mtu anapobeba fedha nyingi mkononi. Ukitumia mfumo huu usalama wa fedha zako unaongezeka maradufu kwa kuwa uhamishaji wa fedha unafanyika kimtandao zaidi.

Faida nyingine ni malipo kufanyika kwa haraka. Mfumo huu ni wa haraka na kuaminika zaidi kutokana na uwekezaji wa teknolojia iliyotumika ambayo inasaidia uhamishaji wa fedha kwa muda mfupi.

Jambo la tatu ni ufanisi wa mfumo wenyewe. Ukitumia mfumo huu unakuwezesha kufanya malipo ya watu wengi kwa wakati mmoja bila ya matatizo yoyote. Ni jambo tu dakika kadhaa, ambapo unaweza kulifanya popote pale ulipo.

Nini kiliwasukuma kuanzisha mfumo huu wa malipo wa Bulk Mobile Payment?

Hapo awali tulikuwa tunaelekeza nguvu zetu zote kwa mteja mmoja mmoja ambaye anatumia huduma hii kwa kuhamisha fedha zake kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye simu yake ya mkononi.

Baadae tukaja kugundua kuwa hatukuwa tukiwatendea haki wateja wa makapuni makubwa (corporate clients) kwa sababu ukiangalia kwa makini utagundua kuwa hawa wateja wakubwa wanaweza kuwa na wafanyakazi wao wanataka kuwalipa ambao yumkini wapo maeneo ya vijijini ni vigumu wao kumfikia kila mmoja.

Tukizungumzia wazo la kuanzisha mfumo huu lilikuja rasmi mwaka 2017 na punde tulianza kulifanyia utafiti na baada ya kukamilisha, mwaka 2018 mwezi Oktoba ndipo tulipoanza utekelezaji wake rasmi.

Mpaka sasa mna wateja wangapi ambao wanatumia mfumo huu wa malipo? Na mapokeo yako vipi?

Kusema kweli watumiaji wa mfumo huu wapo wengi sana ila sitaweza kuwataja ni wangapi. Kwa msisitizo tu kuwa kama Benki licha ya kuwa na watumiaji wengi lakini bado hatujafikia kule tunapopataka ndiyo maana tunaendelea kuhakikisha tunawafikia hadi wale ambao wako mbali nasi.

Kwa upande wa mapokeo, kwa kweli yanatia moyo. Watu wengi wameonyesha kufurahishwa na mfumo huu namna unavyofanya kazi pengine kinyume na matarajio ya wengi. Na hii ni kwa sababu wateja wanaona hawalazimiki kuja mpaka benki badala yake wanaweza kufanya miamala wakiwa katika maeneo yao.

Changamoto gani ambazo mmekuwa mkikabiliana nazo?

Changamoto pekee inayopatikana hapa ni kushindwa kuutumia mfumo huu wakati ukiwa umewekwa kwa ajili ya matumizi ya wateja. Mteja anapokuwa na mtandao wenye nguvu mfumo huu hufanya kazi vyema. Makampuni yanatakiwa kuwa na taarifa sahihi na zilizohakikiwa ili kuweza kufanya malipo hayo.

Nini matarajio yenu juu ya mfumo huu? Na mnajiona wapi baada ya miaka mitano?

Kikubwa ni kuongeza idadi ya wateja wengi watakaokuwa wakitumia mfumo huu. Na nipende kuwahakikishia kuwa watakapofika kwetu watapata huduma zaidi ya hii. Tunakoelekea siyo pabaya sana, miaka mitano ijayo ninatumai teknolojia itakuwa imeshapiga hatua na pengine mfumo huu kwa mda huo utakuwa umeimarika maradufu.

Mna ujumbe gani kwa wadau, wateja na Watanzania kwa ujumla?

Ujumbe wangu unakwenda kwa wateja wetu na hata wale wasio wateja wetu wajaribu kutumia mfumo wa Bulk Mobile Payment. Tumeona namna ambavyo mfumo huu umeweza kuwasaidia wateja wetu hususan makampuni ambayo yameajiri vibarua kufanya malipo yao baaada ya kazi kukamilika.

Share.

About Author

Leave A Reply