Monday, June 17

Aussems achekelea Yanga kupoteza Iringa

0


By Khatimu Naheka

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema mchezo wao wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting hatawatumia wachezaji walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars, huku akifurahi kwa wapinzani wao Yanga kupoteza kitawapa morali zaidi.

Aussems amesema kuelekea mechi hiyo atabadili sura ya kikosi chake akiwa na mchanganyiko ya baadhi ya waliocheza mechi ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa na wale ambao hawakucheza kabisa.

Kocha huyo amesema ingawa wanatambua ugumu wa mechi hiyo, lakini kitendo cha wapinzani wao katika mbio za ubingwa Yanga kupoteza dhidi ya Lipuli kimewapa morali zaidi ya kushinda mechi hiyo.

Amesema watatumia matokeo mabaya ya Yanga kupata morali zaidi ya kupata ushindi dhidi ya Ruvu ili wazidi kuwakimbia katika kupunguza viporo vyao.

Hata hivyo, Aussems ameonyesha wasiwasi kwa wachezaji wake waliopo katika kikosi cha Stars baada ya kusikia wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku.

Mbelgiji huyo amesema ratiba hiyo inafanyika kweli wasiwasi inaweza kuwachosha zaidi vijana wake ambapo maombi yake ni kuona wachezaji wake hao wanarudi wakiwa katika hali nzuri.

Share.

About Author

Leave A Reply